• Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • Instagram
  • Youtube

Sunday, 23 August 2015

Pedro Rodriguez atua rasmi Chelsea

Klabu ya Chelsea imeipiku Manchester United katika mbio za kumsajili Pedro Rodriguez, 28, aliyekamilisha uhamisho wake kutoka Barcelona kwa ada ya ya pauni mil 21.1 na mkataba wa miaka minne ndani ya Chelsea.
PEDRO3
Pedro akiwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Cesc Fabregas
Baada ya uhamisho huo kukamilika Pedro aliwajulisha mashabiki kwa tweet ya kuishukuru klabu ya Barcelona na pia akielezea furaha yake ya kujiunga na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza.
“Naishukuru klabu ya Barcelona pamoja na Chelsea kwa kufanikisha uhamisho huu, ninatazamia kuendelea kushinda vikombe na klabu Chelsea,” alisema Pedro.
ped3
Vikombe ambavyo Pedro amewahi kushinda akiwa na klabu ya Barcelona
PEDRO4
Pedro akifanya mazoezi na mlinzi wa Chelsea Cesar Azpilicueta kwenye uwanja wa Cobham

Contact

Get in touch with me


Adress/Street

12 Street West Victoria 1234 Australia

Phone number

+(12) 3456 789

Website

www.johnsmith.com